Description
Bembea ya Maisha ni hadithi kuhusu Yona na mkewe Sara pamoja na Bunju na mkewe Neema. Wahusika hawa wanajikuta katika vuta n?kuvute inayochochewa na mitazamo ya kitamaduni, uhalisia wa mambo pamoja na matamanio ya wahusika binafsi. Baina yao kuna mitikiso inayotishia familia, ndoa na mahusiano ya kijamii. Kuna shutma, shaka, tuhuma na mivutano. Lakini pia kuna hongera, imani, ushirikiano, upendo, kutanabahi na mshikamano. Katika huu mseto wa mambo ipo sauti imara ya Sara inayosikika ikihimiza na kuzindua. Sauti inayoiona kila hali mfano wa bembea.
Reviews
There are no reviews yet.